Tuesday, September 28, 2021


 


BAADA ya kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wameomba msamaha kwa kilichotokea Uwanja wa Mkapa.


Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes haikuwa na bahati mbele ya Yanga baada ya kuokota bao dakika ya 10 nyavuni likadumu mpaka dakika ya 90.

Shomari Kapombe,  nahodha msaidizi wa Simba amesema kuwa hawakupanga kupata matokeo hayo ila imetokea bahati mbaya jambo ambalo wanaomba msamaha.

"Mchezo wetu uliopita hatukupanga kupoteza ila imetokea hivyo hakuna namna, kila mchezaji ameumia na tunatambua kwamba mashabiki wameumia kwa kilichotokea tunaomba msamaha.

"Kwa mashabiki waendelee kuwa pamoja nasi kwani kazi bado inaendelea na kuelekea kwenye mchezo wetu wa kesho dhidi ya Biashara United tuna amini kwamba tutapata matokeo," amesema.

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa matokeo ya mchezo uliopita hawakuyatarajia hivyo wanajipanga kwa ajili ya mchezo wa kesho.

Simba itamenyana na Biashara United kesho kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni msimu wa 2021/22.

0 comments:

Post a Comment