MLINZI wa Kulia wa Simba Shomari Kapombe, ataukosa mchezo wa leo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma Jiji, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma saa 10:00 jioni.
Kocha msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema ukimuacha Kapombe wachezaji wengine wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa huo ambao wanaamini utakuwa mgumu.
“Tunahitaji alama tatu kwenye mchecho kutokana na matokeo ya mechi zetu tatu zilizopita ili kurudisiha ari kikosini pamoja na hamasa kwa mashabiki”.
Beki huyo mwenye uwezo mkubwa wa kupanda na kushuka ataukosa mchezo huo kwa sababu ya majeruhi aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Biashara United.
Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Karume, Mara ubao ulisoma Biashara United 0-0 Simba na kuzifanya timu hizo kugawana pointi mojamoja.
Wanakutana na Dodoma Jiji ambayo imetoka kufungua pazia la ligi kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.
0 comments:
Post a Comment