Monday, October 25, 2021

 

MABINGWA watetezi, Manchester City jana wameibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Brighton & Hove Albion Uwanja wa The AMEX.
Mabao ya Man City yalifungwa na Ilkay Gundogan dakika ya 13, Phil Foden mawili dakika ya 28 na 31 na Riyad Mahrez dakika ya 90 na ushei, wakati bao pekee la Alexis Mac Allister dakika ya 81 kwa penalti.
Man City inafikisha pointi 20 na kusogea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili na vinara, Chelsea, wakati Brighton inabaki na pointi zake 15 katika nafasi ya nne baada ya timu zote kucheza mechi tisa.

 

0 comments:

Post a Comment