Monday, October 18, 2021

 



TIMU ya Geita Gold imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya Jumamosi Uwanja wa Nyankumbu, Geita.
Danny Lyanga alianza kuifungia Geita Gold dakika ya 47, kabla ya Boban Zirintusa kuisawazishia Mtibwa Sugar dakika ya 64 katika mchezo ambao kila timu ilipoteza mkwaju wa penalti.
Na Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera Sugar ililazimishwa sare ya bila kufungana na Mbeya City.

0 comments:

Post a Comment