Real Madrid huenda wakafufua azma yao wa kumsaka mshambuliaji wa Manchester United na Uruguay Edinson Cavani, 34, dirisha la uhamisho litakapofunguliwa tena mwezi Januari. (El Nacional -kwa Kihispania)
Chelsea bado wanajadiliana na wakala wa beki wa Ujerumani Antonio Rudiger, 28, kuhusu mkataba mpya. (Fabrizio Romano via Twitter)
Kiungo wa kati wa England Kalvin Phillips anakaribia kutia saini mkataba mpya na Leeds- kama anavyosema wakala wa mchezaji huyo wa miaka 25- pande zote "ziko tayari" kufanikisha mpango huo. (John Percy via Telegraph)
Mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 25, ataangalia tena mustakabali wake katika klabu y Chelsea ikiwa atashindwa kurudi katika timu ya Thomas Tuchel - na huenda akarejea Ujerumani mwisho wa msimu huu. (Telegraph - usajili unahitajika)
Barcelona haitamfuta kazi mkufunzi wake Mholanzi Ronald Koeman kabla ya kukipiga na mabingwa wa La Liga Atletico Madrid Jumamosi hii. (Sport)
West Ham huenda wakapata nafsi ya pili ya kumsaini Luca Pellegrini, 22, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia akijizatiti kupata nafasi ya kuchezea Juventus. (Calciomercato -kwa Kitaliano)
Mshambuliaji wa Arsenal Eddie Nketiah, 22, anataka kuondoka Gunners, huku klabu za Leeds, Aston Villa na Brentford zote zikifuatilia hali ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England wa chini ya miaka -21 international. (Ekrem Konur via Twitter)
Mkufunzi wa Liverpool Jugen Klopp anataka kumsaini winga wa Bayern Leverkusen na Ufaransa Moussa Diaby, 22. (Calciomercato - kwa Kitaliano)
Paris St-Germain ilimtaka kiungo wa kati wa Liverpool na England Jordan Henderson, 31, kabla wafanikiwe kumsajili Lionel Messi, 34, kwa uhamisho wa bure kutoka Barcelona msimu huu. (Here We Go podcast via GMS)
Tamko la afisa mkuu mtendaji wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke, la kupuuza ripoti kwamba mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 21, ana 'makubaliano ya uhamisho' na klabu hiyo, limemkasirisha wakala Mino Raiola. (AS)
Barcelona wanamsaka kinda wa Uswidi Williot Swedberg, 17. Kiungo huyo wa kati pia ananyatiwa na klabu za Liverpool na AC Milan. (Fichajes -kwa Kihispania)
Steve Bruce amewaambia marafiki zake kuwa anajiskia "mnyonge" na anafikiria kuachana na Newcastle kama kocha wao kwa mara ya kwanza. (Football Insider)
0 comments:
Post a Comment