Wednesday, October 20, 2021

 

j

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Chelsea wako tayari kumfanya kiungo wake wa England Mason Mount kuwa mmoja wa wanaolipwa zaidi wakati klabu hiyo ikijiandaa kuanza mazungumzo ya mkataba mpya na nyota huyo mwenye miaka 22. (Goal)

Mshanbuliaji wa Hispania Ansu Fati, 18, amakaribia kusaini mkataba mpya wa muda mrefu kusalia Barcelona kukiwa na kipengele cha ada ya £846m) akitaka kuo doka kama ikivyo kwa nyota mwenzake wa Hispania Pedri, 18. (Fabrizio Romano via Twitter)

Beki wa kulia wa Atletico Madrid na England Kieran Trippier, 31, ambaye alikua akihusishwa sana na mipango ya kuhamia Manchester United katika majira ya joto, anasema angelipenda kucheza ligi kuu ya England kwa mara nyingine. (Mirror)

Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer ana mpango wa kuondoa angalau wachezaji watano dirisha la Januari likifunguliwa. (Sun)

Klabu za Liverpool, Borussia Dortmund au RB Leipzig zitapaswa kulipa kati ya 30m na 40m euros kupata saini ya mshambuliaji wa RB Salzburg na Ujerumani Karim Adeyemi, 19. (ORF - in German)

as

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Wamiliki wapya wa Newcastle hawajazungumza bado na kocha Steve Bruce baada timu hiyokuchapwa na Tottenham Hotspurs Jumapili. (Daily Star)

Mlinzi wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 22, hana furaha pale Juventus, hali inayomsukuma wakala wake Mino Raiola kufanya mazungumzo na Barcelona kuhusu uwezekano wa kuhamia huko. (Sport - in Spanish)

Mshambuliaji wa FC Dallas na Marekani Ricardo Pepi ameviweka masikio juu vilabu vikubwa Ulaya zikiwemo vya Liverpool na Bayern Munich kwa kuomba kuondoka rasmi klabuni- lakini kinda huyo mwenye miaka 18 ameshakubaliana malipo binafsi ikiwemo mshahara na klabu Wolfsburg. (CBS Sport)

Aston Villa itapaswa kuharakisha kumsaini nyota wa River Plate Julian Alvarez kwakuwa klabu ya ligi kuu Italia (Serie A) ya AC Milan wanamtaka pia mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 21. (Calciomercato - in Italian)

Klabu za Newcastle United Leeds United zitamkosa kiungo wa Blackburn Rovers muingereza Joe Rothwell baada ya nyota huyo mwenye miaka 26 kuamua kusaini klabu ya Rangers. (TEAMtalk)

West Ham United wanamfuatilia mlinda mlango wa Barcelona Neto, 32, ambaye atakua tayari kusaini mkata wa mkopo na kuondoka Nou Camp mwezi Januari iwapo klabu itakayomsajili itakubali kumsajili mbrazil huyo moja kwa moja katika dirisha kubwa la usajili la majira ya joto. (Sport - in Spanish)

0 comments:

Post a Comment