HAJI Manara Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa watapambana na Geita Gold kwa heshima licha ya kwamba imepanda daraja msimu huu.
Manara amesema baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao walifanikiwa kuondoka na alama tatu kwa ushindi wa bao 1-0 wanaelekeza nguvu katika mchezo wa kesho dhidi ya Geita Gold.
"Tunakwenda hatua kwa hatua,hatutasema sana zaidi ya hamasa kwa watu wetu.Mchezo wa Kagera Sugar umepita, kwa sasa tunachoangalia ni mchezo dhidi ya Geita Gold.
"Ni muhimu sana kwa kuwa ni mchezo wa kwanza nyumbani katika msimu huu. Haijalishi kwamba wamepanda daraja msimu huu lakini tunao wajibu wa kuwaheshimu kama timu ya ligi. Lakini wanapaswa kujua wanakuja kucheza na Yanga," amesema Manara.
Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Nasreddine Nabi kipo Dar es salaam tayari kuwakaribisha Geita Gold kesho kwa Mkapa.
0 comments:
Post a Comment