Monday, November 8, 2021

 



BAO pekee la Emile Smith Rowe dakika ya 56 limeipa Arsenal ushindi wa 1-0 dhidi ya Watford katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
Arsenal ingeweza kuondoka na ushindi mpana kama si kipa wa Watford, Ben Foster kuokoa penalti ya Nahodha, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 36.
Watford ilimaliza pungufu baada ya Juraj Kucka kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 89 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea rafu Nuno Tavares.
Arsenal inafikisha pointi 20 baada ya ushindi huo katika mchezo wa 11 na kujivuta nafasi ya tano sasa ikizidiwa pointi sita na vinara, Chelsea.

0 comments:

Post a Comment