Tuesday, November 23, 2021

 



KLABU ya Yanga imekubaliana na maamuzi ya Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) kutupilia mbali kesi yao dhidi ya winga Mghana, Bernard Morrison.
“Matokeo ya kesi hii hayatoirudisha nyuma klabu ya Yanga katika kupambania haki zake pale itakapoona inafaa kufanya hivyo,”imesema taarifa ya Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla.
Mapema leo taarifa ya CAS ilisema kwamba mkataba wa awali wa Yanga na Morrison ulimalizika Julai 14, mwaka 2020 na wa pili ambao Mghana huyo anaukana alisharejesha fedha za klabu hiyo dola za Kimarekani 30,000 hivyo hakuna kesi baina yao.

0 comments:

Post a Comment