Friday, December 31, 2021

 


Sanamu ya Cristiano Ronaldo in Goa, Indias

CHANZO CHA PICHA,@MICHAELLOBO76

Maelezo ya picha,

Wakosoaji wanasema magwiji wa soka nchini wanapaswa kutambuliwa katika jimbo la Goa nchini India

Sanamu mpya ya nyota wa soka wa Ureno Cristiano Ronaldo imepokelewa kwa hisia mseto nchini India.

Sanamu hiyo imewekwa katika jimbo Goa magharibi, ambako mchezo wa soka ni maarufu sana, maafisa wanatumai maafisa wanatumai itawatia moyo vijana.

Lakini Goa pia ni koloni la zamani la Ureno, na ni miaka 60tangu jimbo hilo lilipokomboloewa kutoka kwa Ureno.

Wakosoaji wanasema wachezaji nyota wa soka wa nchi hiyowanastahili kutambuliwa,hasa ikizingawa wachezaji kadhaa wa zamani na wa sasa wa timu ya taifa ya India ni Wagoa.

"Nimesikitika sana kusikia sanamu ya Ronaldo imezinduliwa nchini. Tujifunze kujivunia sanamu za nyota wetu kama Samir Naik na Bruno Coutinho,"Wakazi wa Goa waliambia shirika la habari la IANS.

Wakati wa uzinduzi wa sanamu hiyo, baadhi ya watu walipeperusha bendera nyeusi wakipinga, gazeti la Times nchini India liliripoti.

Timu ya soka ya Ureno ni maarufu sana katika jimbo la Goa, na kwa sababu ya ukoloni wake wa zamani, wenyeji wengi wameishi Ureno au wana familia huko.

Lakini baadhi ya watu katika jimbo hilo la India wanahisi ni makosa kuweka sanamu hiyo wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya Goa kupata uhuru wake kutoka kwa Ureno, ambayo ilifanyika miaka 14 baada ya sehemu zingine za India zilizobaki kukombolewa kutoka kwa utawala wa Waingereza.

"Kuweka sanamu ya mwanasoka wa Ureno mwaka huu ni kufuru. Tunalaani hili," IANS ilimnukuu mwanaharakati wa mrengo wa kulia Guru Shirodkar akisema.

Kuna wapigania uhuru wengi huko Goa ambao wametukanwa," aliongeza.

Michael Lobo, mbunge wa eneo hilo katika chama tawala cha Bharatiya Janata Party (BJP), aliweka picha yake kwenye ukurasa wa Twitter akiwa na sanamu hiyo, akisema kwamba ilikuwa imewekwa "kwa ombi la vijana wetu" ili kuwatia moyo "kupandisha viwango vya soka " .

Ingawa kriketi inasalia kuwa mchezo maarufu zaidi wa India, kandanda - haswa Ligi Kuu ya Uingereza - inapendwa katika maeneo kadhaa ya nchi - Kerala kusini, Goa magharibi, Bengal Magharibi mashariki na majimbo yote manane ya kaskazini-mashariki

Cristiano Ronaldo, ambaye kwa sasa anachezea Manchester United, anapendwa na mashabiki wengi na anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora katika historia ya mchezo huo.

Mshambuliaji huyo wa miaka 36- hajatoa tamko lolote kuhusiana na sanamu hiyo.

Hii sio mara ya kwanza kwa sanamu yake kuibua hisia - mnamo 2017 sanamu ya ajabu ya Ronaldo ilidhihakiwa na hatimaye kubadilishwa katika uwanja wa ndege wa Madeira nchini Ureno.

0 comments:

Post a Comment