Friday, December 31, 2021

 



WENYEJI, Namungo FC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Namungo FC walitangulia kwa bao la mshambuliaji wake tegemeo, Relliant Lusajo dakika ya 10, kabla ya Dennis Nkane kuisawazishia Biashara United dakika 37.
Kwa sare hiyo kwenye mchezo wa 11 kwa wote, Namungo FC wanafikisha pointi 13 katika nafasi ya nane, wakati Biashara wanafikisha pointi tisa katika nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.

0 comments:

Post a Comment