Sunday, January 2, 2022

 

Mohamed Salah, Sadio Mane, Edouard Mendy, Pierre-Emerick Aubameyang, Maxwel Cornet

CHANZO CHA PICHA,REUTERS/EPA

Maelezo ya picha,

Sadio Mane, Mohamed Salah, Edouard Mendy, Pierre-Emerick Aubameyang, Maxwel Cornet na wengine wengi wataondoka kwa wiki kadhaa

Wachezaji soka wa Afrika sasa wanaweza kuchezea klabu zao hadi Januari 3 kabla ya kwenda kuwakilisha nchi zao katika Kombe la Mataifa ya Afrika, linasema Shirikisho la Soka Afrika.

Sheria za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) zinasema kuwa Klabu zinapaswa kuwaachilia wachezaji Disemba 27 kwa michuano hiyo, ambayo inaanza Januari 9 .

Lakini barua kutoka FIFA kwa Jukwaa la Ligi za Dunia ilisema Caf imekubali wachezaji wanaweza kucheza rasmi katika vilabu vyao hadi Januari 3.

"Uamuzi huu unachukuliwa kwa nia njema na mshikamano," Fifa ilisema.

Inamaanisha kuwa Liverpool wataweza kuwa na mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, winga wa Senegal Sadio Mane na kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita kwa mchezo wao wa Januari 2 huko Chelsea, ambao watakuwa na kipa wa Senegal Edouard Mendy.

Wachezaji wa Algeria Riyad Mahrez na Said Benrahma wanaweza kuchezea Manchester City na West Ham mtawalia, huku wengine pia wakinufaika.

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika itaendelea hadi Februari 6, huku Leeds United, Newcastle United, Norwich City na Tottenham zikiwa ni timu pekee za Ligi ya Premia ambazo hazijapoteza mtu yeyote kwa dimba hilo.

Katika barua kutoka kwa naibu katibu mkuu wa Fifa Mattias Grafstrom kwa Jukwaa la Ligi za Dunia na kambi za Ligi za Ulaya, bodi inayosimamia soka duniani ilisema uamuzi huo umechukuliwa "pamoja na vilabu vilivyoathiriwa kwa kutambua ukweli kwamba wao, kama wadau wote wa mchezo wa soka, wameathiriwa vibaya na janga la Corona.

Aliongeza: "Pia inachukuliwa kuwa roho ya ushirikiano wa pande zote inabaki kati ya Caf na wadau wote wanaohusika katika suala hili, ikiwa ni pamoja na kuhusiana na kuachiliwa kwa wachezaji na utoaji wa misamaha ya michezo kwa usafiri na vikwazo vya karantini ikiwa itahitajika katika siku zijazo."

Aliongeza: "Pia inachukuliwa kuwa moyo wa ushirikiano wa pande zote inabaki kati ya Caf na wadau wote wanaohusika katika suala hili, ikiwa ni pamoja na kuhusiana na kuachiliwa kwa wachezaji na utoaji wa msamaha ya michezo kwa usafiri na vikwazo vya karantini ikiwa itahitajika katika siku zijazo."

0 comments:

Post a Comment