Saturday, January 15, 2022

 



KLABU ya Simba imetangaza rasmi kumrejesha kiungo wake Mzambia, Clatous Chotta Chama baada ya nusu msimu tangu aondoke kwenda RS Berkane ya Morocco.
Agosti mwaka jana Simba ilimuuza Chama RS Berkane kwa dau la Sh. Bilioni 1.5, lakini ndani ya nusu mwaka Mzambia huyo ameshindwa kumshawishi kocha Mkongo, Florent Ibengé.
Chama mwenye umri wa miaka 30 sasa, aliibukia Nchanga Rangers FC mwaka 2013 kabla ya kwenda ZESCO United hadi 2017 alipohamia Ittihad ya Misri, alikocheza kwa msimu mmoja kabla ya kurejea Zambia kujiunga na Lusaka Dynamos na mwaka 2018 akajiunga na Simba.


0 comments:

Post a Comment