Saturday, January 15, 2022

 



KLABU ya Yanga imemtambulisha beki Ibrahim Abdallah Hamad ‘Bacca’ kutoka KMKM ya Zanzibar kuwa mchezaji wake mpya wa tano dirisha hili dogo, wote wazawa.
Bacca aliibukia Official page of Ibrahim Abdalla Hamad timu ya watoto ya Mapembeani, kabla ya kwenda Real Kids, baadaye Taifa Jang’ombe, Malindi na KMKM ambako baada ya kung’ara kwenye Kombe la Mapinduzi anatua Jangwani.
Wachezaji wengine waliosajiliwa Yanga dirisha hili dogo ni kipa Abdallah Mshery kutoka Mtibwa Sugar, kiungo Salum Abubakar ‘ Sure Boy’ kutoka Azam FC, winga Dennis Nkane kutoka Biashara United na mshambuliaji Crispín Ngushi kutoka Mbeya Kwanza.

0 comments:

Post a Comment