Inaonekana wachezaji wa kibrazil wamekuwa wepesi kuzungumzia matamanio yao ya kujiunga na Manchester United hadharani katika siku za hivi karibuni.
Wiki
iliyopita alikuwa Anderson Talisca, alipokuwa akiongea na Globo
Esporte, alipoulizwa kuhusu kocha wa United, Jose Mourinho alisema
angependa kumtumikia Jose na anaamini kuna uwezekano uhamisho wa kwenda
United utawezekana.Na jana ilikuwa zamu ya kiungo wa Monaco, Fabinho kumzungumzia Mourinho na Manchester United. Fabinho alikuwa akihojiwa na na Esporte Interativo, na alipoulizwa atasijikiaje kuhusu kuhamia Manchester United ikiwa wakileta ofa rasmi.
Fabinho akajibu:
“Litakuwa jambo lenye majaribu makubwa. Kwanza nitazungumza na wakala
wangu, timu yangu Monaco, ili niweze kuamua kila kitu vizuri. United ni
klabu kubwa hivyo itanibidi nifikirie vizuri kuhusiana na hilo.” Jana Alhamisi gazeti kubwa la nchini Italia Corriero Dello Sport liripoti kwamba United imekubaliana na Monaco kulipa kiasi cha €35m + €5m za bonasi ili kumsaini kiungo huyo wa Monaco mwenye umri wa miaka 23.
.

0 comments:
Post a Comment