MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Chile anayekipiga katika klabu
ya Arsenal ya Uingereza, Alexis Sanchez anatajwa kuwa amekubali kujiunga na
klabu ya Manchester City.
Mwandishi mmoja wa
habari ambaye ni rafiki mkubwa wa mwanasoka huyo amesema LEO kwamba ameambiwa
“laivu” na Sanchez kwamba anaondoka rasmi na chaguo lake ni Manchester City.
Gerard Romero ambaye
ni mwandishi wa habari raia wa Hispania amesema kwamba ameambiwa na sanchez
kwamba anakwenda Man City ili kuungana na kocha wakw wa zamani Pep Guardiola.
Arsenal imekuwa kwa muda mrefu sasa ikihaha kumbakiza mchezaji huyo katika
kikosi chake, lakini kwa tarifa hizo mpya ni kama vile jitihada hizo zimekwama.
Nyota huyo mwenye
umri wa miaka 28 amekuwa na msimu bora katika Arsenal chini ya kocha wake,
Arsene Wenger na ametumbukiza kambani mabao 30 katika mechi zote za mashindano.
Hata hivyo, winga huyo yuko nje ya mkataba msimu ujao na kama anaondoka kwenda
Man City maana yake anaondoka akiwa kama mchezaji huru. Na kwa mujibu wa
Romero, tayari mazungumzo ya uhamisho wake yanaweza kuanza wakati wowote ili
kujua ni kiasi gani arsenal inaweza kumpa kutokana na muda mdogo wa mkataba
wake uliobaki.
Mwandishi huyo
ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Alexis Sanchez amekamilisha uhamisho
wake kwenda man City. Manchester na Arsenal wameridhia uhamisho wake.” Wiki
iliyopita Sanchez ameiambia Arsenal kwamba hana haraka ya kujadili kuhusu
mkataba mpya mpaka baada ya mashindano ya Kombe la mabara.
Pep Guardiola amekuwa katika mawindo makali ya kusaka
wachezaji wa maana kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment