
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund
Pierre-Emerick Aubameyang hatouzwa katika majira haya ya kiangazi na
atasalia katika timu yake.
Mkurugenzi wa Dortmund Michael Zorc,
amethitibisha kuwa mchezaji huyo anayewinda na vilabu vya Paris
St-Germain , AC Milan na Chelsea haendi kokote."Tumeshaamua kwamba Auba atabaki hapa kuendelea kuitumikia timu hii." Alieleza Mkurugenzi huyo.
Aubameyang msimu uliopita aliifungia timu yake jumla ya mabao 31 na kuisaidia kutwaaa taji la kombe la Ujeruman, na kumaliza katika nafasi ya tatu katika ligi ya Bundasliga.
0 comments:
Post a Comment