
Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio
Conte amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuwanoa mabingwa
watetezi wa taji la ligi kuu ya England.
Conte katika msimu wake
wa kwanza ameisadia Chelsea kutwaa ubingwa wa England kwa kushinda
michezo 30,na kucheza fainali ya michuano ya kombe la Fa licha ya
kufungwa na Arsenal katika fainali.Baada ya kusaini mkataba huo mpya Conte alisema " nina furaha sana kwa kusaini mkataba huu mpya,"
Nae mkurugenzi wa klabu hiyo Marina Granovskaia, aliongeza kwa kusema "mafanikio makubwa waliyopata, pamoja na uhodari wa kocha huyo ndio kimewapa imani ya kumuongezea Conte mkataba mpya".
0 comments:
Post a Comment