
Manchester United wamekamilisha
ununuzi wa kiungo wa kati wa Serbia Nemanja Matic kutoka kwa mabingwa
wa Ligi ya Premia Chelsea kwa £40m.
Mchezaji huyo ametia saini mkataba wa miaka mitatu.Matic, 28, amekuwa mchezaji wa tatu kununuliwa na United majira haya ya joto.
United walikuwa wamemnunua beki Victor Lindelof kwa £31m kutoka Benfica na kisha wakalipa £75m kumchukua Romelu Lukaku kutoka Everton.
Meneja wa United Jose Mourinho alimweleza Matic kama mchezaji anayecheza vyema na wenzake kwenye timu na "ana kila kitu ambacho tungetaka katika mwanakandanda; uaminifu, uendelevu na kuwa na ndoto kuu".
Matic amesema ana furaha sana kujiunga na United wakati huu wa kusisimua.
Mourinho, alipokuwa Chelsea, alitumia £21m kumnunua Matic kutoka Benfica kwa kipindi cha pili Stamford Bridge Januari 2014.
Matic alifunga bao moja katika mechi 35 alizochezea Chelsea Ligi ya Premia msimu wa 2016-17, ambapo pia alifunga bao la kipekee wakati wa ushindi wao nusufainali Kombe la FA dhidi ya Tottenham Aprili.
0 comments:
Post a Comment