
Wageni wa Ligi Kuu ya Tanzania
bara timu ya Lipuli FC imewasajili kwa Mkupuo wachezaji wawili ambao
walishawahi kuchezea Yanga ambao ni mshambuliaji Malimi Busungu ambaye
amesaini mwaka mmoja pamoja kiungo mshambuliaji Omega Seme ambaye naye
mwaka mmoja.
Lipuli Fc iliyochini ya kocha
Selemani Matola imeanza usajili wa nguvu kwa ajili ya kukabiliana na
Mzunguko wa Ligi Kuu ya Vodacom inayotarajia kuanza Agosti 26.
Lipuli toka Iringa msimu ujao
itatumia uwanja wake wa Nyumbani wa Samora na imecheza mchezo na Azam Fc
na kufungwa magoli 4-0 kabla ya kuzinduka na kuifunga Singida United
goli 1-0 yote michezo ya kirafiki.
0 comments:
Post a Comment