
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi
ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA), Ramadhani
Mambosasa ametangaza orodha ya majina sita ya mwisho ya wagombea nafasi
mbalimbali katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.
Kwa mujibu Mambosasa, wagombea
hao kwa sasa hawana budi kuendelea na kampeni hadi Agosti 9, mwaka huu
ambako uchaguzi huo umepangwa kufanyika kufanyika Agosti 10, mwaka huu
mjini Dodoma.
Waliopitishwa katika orodha ya
mwisho kuwania nafasi mbalimbali za uongozi – ngazi ya taifa ni pamoja
na Kidao Wilfred, Lister Manyara, Michael Bundala, Dismas Haonga,
Jamhuri Kihwelo, George Komba, Samuel Moja na Maka Mwalwasi na Mohammed
Tajdin.
Nafasi zinazowaniwa ni
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka
Hazina, Wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
0 comments:
Post a Comment