Thursday, August 3, 2017

Picha kubwa wachezaji wa Atletico Madrid wakifurahia na Kombe la Audi baada ya kuifunga Liverpool (picha ndogo juu kushoto) kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 usiku wa jana Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich, Ujerumani. Keidi Bare alianza kuwafungia wenyeji dakika ya 33, kabla ya Roberto Firmino kuwasawazishia wageni dakika ya 83 na katika mikwaju ya penalti waliofunga na Atletico ni Griezmann, Torres, Gabi, Gaitan na Luis wakati za Liverpool zilifungwa na Firmino, Origi, Kent na Grujic huku Henderson akikosa

0 comments:

Post a Comment