Kocha
Mkuu wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa kikosi chake
kinaweza kushinda ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza baada ya msimu
uliopita kufanya vibaya na kumaliza kwenye nafasi ya nne ambayo imewapa
nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.
Liverpool ilianza msimu wa 2016-17
vizuri na walikuwa pointi sita pekee nyuma ya viongozi na hatimaye
bingwa wa ligi Chelsea mnamo mwezi Januari.
Lakini walirudi nyuma baada ya
kupata ushindi mmoja mwezi Januari na Februari kabla ya kumaliza katika
nafasi ya nne pointi 17 nyuma ya Chelsea.
”Tutashiriki mechi za ubingwa.hatutaki kuanza msimu bila kuwa na lengo lolote”, alisema Klopp.
“Lazima tuwe na lengo na nadhani tuna timu nzuri sana sasa.tulikuwa na bahati mbaya msimu uliopita”.
”Nadhani tunaweza kucheza vyema
.Tuwe na matumaini kwamba kila kitu kitakuwa shwari. Klop alisema kuwa
kwamba mchezaji Phillipe Coutinho hauzwi, licha ya Barcelona kumtaka”

0 comments:
Post a Comment