Wednesday, September 13, 2017

Imeandikwa na mshabiki wa soka Tanzania.
Shikamoo Haji, naamini unaendelea vizuri na hongera kwa usajili muliofanya msimu huu hakika ni usajili mzuri na munaonekana wazi mwaka huu munataka kombe, japo kila mwaka mumedai munataka kombe lakini mwisho wa ligi munaambulia maneno.
Safari hii upana wa kikosi chenu ni wazi kwamba Simba munataka ubingwa, na naamini mukiendelea na umoja muliokuwa nao kati ya mashabiki na klabu kwa hakika mutachukua kombe la ligi msimu huu na makombe mengine.
Haji wewe ni mtu mzima na naamini wewe una busara na ndio maana Simba walikuamini na wakakupa usemaji wa klabu, umri wako, busara zako na weledi wako ni kati ya vitu ambavyo Simba walikuamini na kukupa usemaji.
Lakini sasa Manara wewe ni msemaji wa Simba au mpondaji wa Yanga, kipindi hiki si mko katika mchakato wa kubadilisha mfumo wa uendeshaji klabu? Naamini ni kipindi ambacho unatakiwa kufanya sana kazi yako na kuwapa mashabiki wa Simba elimu kuhusu hili.
Lakini naona uko bize sana kuwasema Yanga, ila pia sio mbaya kwani Yanga si ni watani wako?huo ndio utani, lakini je kuanza kuwapa wachezaji wa Yanga majina mara sijui Shilole, uko busy na kuandika vitu ambavyo haviisaidii Simba na sidhani kama ulilipwa kwa ajili ya hilo.
Mbaya zaidi leo nimeona umepost picha kuhusu mwenyekiti wa Yanga ambaye kwa sasa yuko matatizoni, Manji ana watoto na ana familia, sawa yuko matatizoni lakini sisi kama familia ya soka inabidi tuachane na masuala ya kesi yake na tuzungumzie yetu ya soka, Manji yuko matatizoni Haji muache.
Haji umeshawahi kujiuliza kama wewe uko matatizoni na mtu mwenzio wa soka akapost jambo baya kuhusu wewe na akaliunga mkono?hata kama ni kweli wewe ungejisikiaje? Ungejisikia vizuri?masuala ya walioko matatizoni na serikali tuwaachie wao sisi tuzungumzie soka.
Wachezaji unaowasema kwa mabaya wengi wana familia, kibaya zaidi unawasema watu hata hawakujibu, mimi naona hawana muda na wewe au labda wanakudharau (sijui), mimi naona kama wao hawaoni ngoja mimi tu nikuambie kwamba fanya kazi yako hayo mengine waachie mashabiki.
Mwisho nakutakia kila la kheri katika kazi yako, nakutakia kila la kheri katika mchakato munaofunya na mpambane uwanjani mubebe ubingwa naamini safari hii hamtalia na ubingwa wa mezani kama ulivyotudanganya mwaka jana kuwa Fifa watawapa.

0 comments:

Post a Comment