Chelsea wameendeleza rekodi yao nzuri dhidi ya timu za
Hispania ugenini baada ya leo kuipiga Athletico Madrid mabao 2 kwa 1,
Athletico walitangulia kupitia kwa Griezman kabla ya Morata na Batshuayi
kufunga mawili.

Mechi
kati ya Athletico Madrid Vs Chelsea ilikuwa mechi ya kwanza kwa
Athletico kucheza katika uwanja wao mpya wa Wandra Metropolitano katika
champions league, mchezo mwingine wa group C ilikuwa kati ya Quarabag vs
As Roma huku Manolas na Dzeko wakiifungia Roma.

CSKA
Moscow wakiwa nyumbani walikubali kupigwa bao 4 kwa 1 na Manchester
United huku Romelu Lukaku akifunga mara mbili,Martial na Mkhtaryan
walifunga bao moja moja huku la Moscow likifungwa na Kuachev na
kuwafanya United kuongoza kundi A.

Dani
Alves, Neyamar na Edison Cavanni waliuua Bayern Munich bao 3 kwa 0,
huku Celtic wakiwa ugenini wakiifunga Anderchelt 3 huku mabao ya Celtic
yakiwekwa kimiani na Patrick Roberts, Scott Sinclair na Griffiths.

Gonzalo
Higuain na Mario Mandzukic waliisaidia Juventus kupata alama 3 katika
Champions League huku Barcelona wakizidi kujichimbia ugenini baada ya
goli la kujifunga la Sebastian Coates.
0 comments:
Post a Comment