KOcha Mkuu wa Bayern Munich,Carlos
Ancelotti hatimaye kibarua chake kimeota mbawa baada ya kufutwa kazi na
maboss wake hii ni Kufuatia kichapo cha 3-0 dhidi ya PSG , bodi ya
klabu hiyo iliamua kumfuta kazi raia huyo wa Italy ambay alichukua
mahala pake Pepe Guardiola msimu uliopita.
Ancelotti mwenye umri wa miaka 58,
aliisaidia Bayern kushinda taji la Bundesliga, lakini hawakuweza kufika
katika raundi ya muondoano ya kombe la vilabu bingwa pamoja na nusu
fainali ya kombe la Ujerumani.
Naibu meneja Willy Sagnol
ataiongoza klabu hiyo kwa muda Bayern wako katika nafasi ya tatu katika
jedwali la ligi , wakiwa alama tatu nyuma ya Borussia Dortmund ,wakiwa
wameshinda mara nne.
0 comments:
Post a Comment