
Manchester United inapanga kumnunua
Antoinne Griezman kwa kitita cha £88m kutoka Atletico Madrid msimu ujao
baada ya mkufunzi Jose Mourinho kuomba uhamisho huo kukamilishwa (Daily
Express)
Chelsea wanatumai kwamba kiungo wa kati Eden Hazard,
26,ataweka kandarasi ya mkataba mpya ambao utamfanya raia huyo wa
Ubelgiji kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi katika ligi ya Uingereza
kwa £300,000 kwa wiki. (Sun)
PSG itaipiku Manchester City katika kumsajili Alexis Sanchez kwa kumpatia mchezaji huyo wa Arsenal £9m kabla ya kumsajili mnamo mwezi Januari. (El Mecurio, via Sun)
Mkufunzi wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa huenda akamsajili mchezaji mwengine wakati wa dirisha la uhamisho mnamo mwezi Januari ili kuchukua mahali pake Benjamin Mendy , 23, ambaye anauguza jeraha la goti.(Independent)
Manchester United na Arsenal ni miongoni mwa klabu zinazomsaka mshambuliaji kinda wa MK Dons' Dylan Asonganyi. (Daily Mirror)

Real Madrid iko tayari kushindana na wapinzani wao Manchester United katika kumsajili mshambuliaji wa Juventus' Paulo Dybala, 23. (Mundo Deportivo, via Daily Star)
Chelsea wanapigiwa upato kumsajili Edinson Cavani iwapo mshambuliaji huyo wa Uruguay mwenye umri wa miaka 30 ataondoka PSG mnamo mwezi Januari. (Sun)
Winga Antonio Candreva anatarajiwa kuondoka Inter Milan, huku Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte akivutiwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.(Calciomercato, via Daily Star)

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Gary Neville amekiri kwamba alifurahishwa wakati mchezaji mwenza David Becham alipoondoka Old Trafford mwaka 2003 kuelekea Real Madrid. (Manchester Evening News)
0 comments:
Post a Comment