
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), limeongeza juhudi za kufundisha makocha wa mpira wa
miguu hapa nchini ili idadi ya walimu wa mpira wa miguu wanaopaswa
kushiriki kwenye programu za maendeleo ya vijana za mikoa.
Hii ni katika kukidhi malengo ya TFF katika kusimamia maendeleo ya soka la vijana hapa nchini.
Kwa sasa, TFF kwa kushirikiana
na mikoa ya Songwe, Lindi na Kigoma, zinaendeshwa kozi ngazi ya awali
(Preliminary) na ngazi ya kati (Intermidiate).
Katika mkoa wa Songwe kozi ya
ukocha zinazoendeshwa ni kozi ya awali Wilaya ya Songwe inayoendeshwa na
Mkufunzi John Simkoko na kozi ya awali, wilaya ya Tunduma inaendeshwa
na Mkufunzi George Mkisi.
Mkoani Lindi kozi ya awali
ilianza Septemba 11, 2017 katika Wilaya ya Kilwa ikiendeshwa na Mkufunzi
Michael Bundala na mkoani Kigoma kuna kozi mbili zinaendelea.
Moja ni ngazi ya awali inaendeshwa na Mkufunzi George Komba na kozi Ngazi ya Kati inaendeshwa na Mkufunzi Rogasian Kaijage.
0 comments:
Post a Comment