
Michuano ya klabu
bingwa barani ulaya kwa msimu wa 2017/2018, utaanza leo rasmi kwa jumla
ya michezo nane kupigwa katika viwanja mbalimbali.
Katika kundi A
Manchester United watakuwa nyumbani katika dimba la Old Trafford
kuwaalika Fc Basel, huku Benfica wakiwa wenyeji wa Cska Moscow.Michezo ya kundi B Bayern Munich, wataanzia nyumbani nchini Ujerumani, kwa kucheza na wabeligiji wa Anderlecht, nao Celtic wakianza kwa kibarua kizito dhidi ya Paris Saint Germain.
Chelsea ya England wataanza kusaka ubingwa wa ulaya kwa kuwakaribisha Qarabag FK, waitaliano wa As Roma wataanza kwa kukipiga na Atletico Madrid, ikiwa ni michezo ya kundi C.

0 comments:
Post a Comment