Hawa ndio vinara wa michuano ya Champions League katika ligi
kuu Uingereza, hakuna anayewagusa Liverpool kwa idadi ya makombe ya CL
wanayo 5, na leo wanaanza kampeni ya kutafuta kombe la 6
watakapowakaribisha Sevilla katika uwanja wa Anfield.

Sheikh
Mansoor msimu huu kati ya ndoto zake msimu huu ni kubeba ndoo ya
Champions League na uwekezaji wake Man City unaonekana wazi anataka
kombe hili, sasa leo nao wanatupa karata yao ya kwanza wakisafiri hadi
Uholanzi kuifuata Feyenoord.

Monaco
msimu uliopita walicheza vizuri sna katika Champions League lakini
safari hii bila Kylian Mbappe, bila Bernardo Silva, bila Tiomue Bakayoko
wanawafuata Rb Leizpg nchini Ujerumani kwa mchezo wao wa kwanza.
Tottenham ambao hawana rekodu nzuri katika uwanja wa Wembley lazima
watahitaji ushindi ili kuanza kujiweka vizuri katika uwanja huo ambapo
hii leo watawakaribisha wababe wa Ujerumani klabu ya Borussia Dortmund.
Mchezo mwingine katika kundi H ambalo linaonekana kuwa moja ya kundi
gumu itakuwa kati ya mabingwa watetezi Real Madrid ambao wataikaribisha
APOEL Nicosia katika dimba la nyumbani la Santiago Bernabeu.

Fc
Porto watakuwa nyumbanu kuwakaribisha Bestikas, Napoli watawafuata
Shaktar Donetsk huku Maribor nao watakuwa Ljudski Vrt Stadium
kuwakaribisha Spartak Moscow.
0 comments:
Post a Comment