Kwa mara ya kwanza Lioneil Messi anamtungua Buffon, Barcelona
wanaaifunga Juventus bao 3 kwa sifuri huku mabao 2 ya Lioneil Messi
yanamfanya kufikisha idadi ya mabao 59 katika hatua ya makundi tu ya
michuano ya Champions League, Ivan Rakitic alifunga bao lingine la
Barcelona.

Edson
Cavanni naye ameuchukua ufalme wa Zlatan Ibrahimovich ambaye alikuwa na
rekodi ya kufunga mabao 20 katika Champions League lakini sasa Cavanni
anakuwa na mabao 22 baada ya kufunga mara mbili dhidi ya Celtic na kuwa
mfungaji bora wa muda wote wa PSG katika michuano ya Ulaya.

Lakini
pia Kylian Mbappe ambaye alifunga bao la pili naye sasa anakuwa na
mabao 7 katika Champions League mwaka huu na ni Cristiano Ronaldo pekee
mwenye magoli mengi kuliko yeye kwani amefunga mabao 10, huku goli la
Neymar likimfanta kuhusika katika magoli 11 dhidi ya Celtic.

Mabao
hayo na lile la kujifunga la Mikael Lustig liliwafanga PSG kuibuka
kidedea na ushindi wa bao 5 kwa bila ugenini dhidi ya Celtic. As Roma
wakiwa nyumbani walilazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya
Athletico Madrid.
Lukaku alifunga bao lake la 10 katika michuano ya CL hatua ya makundi
huku Fellaini akifunga bao lake la 50 tangu aanze kuchezea ligi kuu ya
Uingereza, bao la tatu la Manchester United liliwekwa kimiani na Marcus
Rashford na mchezo kuisha kwa United kuibuka na ushindi wa bao 3 kwa
nunge dhidi ya Fc Basel.

Chelsea
waliwapiga vibonde Quarabag Fc bao 6 kwa nunge, bao la Cesar
Azipuculeta lilikuwa bao lake la kwanza katika michezo 46 iliyopita
aliyoitumikia Chelsea, mabao mengine ya Chelsea yalifungwa na Bakayoko,
Batshuayi(2), Zapacosta, na Pedro Rodriguez.

Bayern
Munich waliipiga Anderchelt waliocheza pungufu kwa dakika 80 baada ya
Sven Kums kuoneshwa kadi nyekundu dakika ya 11 bao 3 kwa 0 huku Robert
Lewandoski akifunga bao lake la 50 katika michezo 53 aliyoichezea Bayern
tangu msimu uliopita, mabao mengine yalifungwa na Thiago Alcantara huku
Joshua Kimmich akifunga la 3.

Benfika
wakiwa nyumbani walichezea kipigo cha bao 2 kwa 1 toka CSKA Moscow huku
mabao ya Moscow yakifungwa na Timur na Vitinho, Benfika likifungwa na
Saferovic, Olympiacos nao wakiwa nyumbani wakafungamwa 3 kwa 2 na
Sporting CP.
Comments
0 comments:
Post a Comment