Hakuna Novack Djokovick, Andr Murray wala Rodger Federer
unataraji Rafael Nadal angefanya nini katika mashindano ya US Open kama
sio kubeba ubingwa huo kwa mara yake ya tatu.
Ndicho alichofanya Mhispania huyo usiku wa leo katika dimba la Arthur
Ashe Stadium akimfunga Msouth Africa Kelvin Anderson kwa seti 6-3,6-3
na 6-4 katika mchezo uliokuwa wazi kwa Nadal.
Rafael Nadal ilikuwa wazi asingepata upinzani mkubwa kwani wachezaji
wote walioko katika 20 bora ya viwango vya tennis walikuwa wameshatoka
na sasa ilikuwa yeye na mchezaji namba 28.
Baada ya kushinda Grand Slam mwaka 2013 hii ni Grand Slam nyingine
kwa Nadal na inatimiza idadi ya Grand Slam 16 kwa Nadal huku akishinda
mbele ya mashabiki wanaompenda kama mwenyeji wa hapo mjini NewYork.
Nadal sasa anakuwa na US Open 3 na kuwa na Grand Slam 16 akimkaribia
kinara wa Grand Slam Rodger Federer ambaye hadi sasa ameweka kabatini
jumla ya Grand Slam 19.
Monday, September 11, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment