Usajili wao ulithibitisha ni nini wanataka,ilikuwa wazi wanataka heshima kwani usajili wa €200m huku majina makubwa kama Bonucci, Andre Silva, Ricardo Rodriguez,Andrea Conti,Mateo Muscchio ilionesha wazi Ac Millan wamepania.
Maisha yamekwenda lakini kijana mzaliwa wa jiji la Tore Annazuita miaka 27 iliyopita Ciro Immobile aliwaonesha Ac Millan kwamba pesa zao si lolote na hata hakutumia mda mrefu bali sekunde 600 tu zilimtosha

Hii ni mara ya kwanza kuona hattrick katika mchezo kati ya Ac Millan na Lazio tangu Andriy Shevchenko kufanya hivyo mwaka 1999 katika dimba la Stadio Olimpique wakati akiifungia Ac Millan bao kama hizo.
Immobile sio tu kufunga bao hizo 3 kati ya 4 lakini hata bao la 4 la Lazio ni yeye aliyeassist na kuuacha ukuta wa Ac Millan unaoongozwa na beki kisiki Bonucci kutoamini ni nini kinachowatokea.
Immobile ameshawahi kuzichezea Juventus akishindwa kufunga bao hata moja, baadae akaifungia Dortmund bao 3 msimu mzima, wakamuuza Sevilla,akapelekwa Torino alikofunga bao 5 na sasa amerudi Lazio.
0 comments:
Post a Comment