Friday, October 6, 2017

Nadal pia ameshinda vikombe vitatu vya US Open

Image captionNadal pia ameshinda vikombe vitatu vya US Open
Mchezaji namba moja wa Hispania Rafael Nadal amefanikiwa kufika hatua ya robo fainali michuano ya China Open baada ya kumchakaza Karen Khachanov wa Urusi.
Nadal ambaye alishinda taji la tatu la US Open mwezi uliopita ameshinda kwa seti 6-3 6-3.
Nadal mwenye miaka 31 alitawala mchezo huo na kumfunika kabisa Khachanov anayeshikilia nafasi ya 42 duniani.
Katika hatua inayofuata atachuana na John Isner wa Marekani aliyemchapa Leonardo Mayer wa Argentina kwa seti 6-0 6-3.

0 comments:

Post a Comment