Friday, October 6, 2017

Harry Kane alifunga goli dakika ya 90

Image captionHarry Kane alifunga goli dakika ya 90
Timu ya taifa ya Uingereza imefanikiwa kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani nchini Urusi baada ya kuichapa Slovenia 1-0.
Harry Kane ambaye ni nahodha wa Uingereza alisaidia kupatikana kwa goli hilo baada ya kupata pande safi kutoka kwa Kyle Walker dakika ya 90.
Goli hili linakua la 11 katika michezo 22 aliyocheza Kane kwa timu yake ya taifa.
Msimamo wa kundi F
Image captionMsimamo wa kundi F
Kocha wa Uingereza Gareth Southgate amesema kufuzu mapema kwa timu yake ni faida kwani wanaweza kupanga vizuri ni namna gani wataingia katika michuano hiyo mikubwa kwa upande wa soka duniani.
Marcus Rashford na Raheem Sterling walionyesha kiwango safi katika mchezo huo.
Mlinda mlango Joe Hart pia aliweza kuokoa michomo hatari ambayo kama ingeingia ingeichelewesha timu yake kufuzu.

0 comments:

Post a Comment