Lionel Andres Messi Cuccittini, jina la mwanasoka anayetajwa kuwa bora wa wakati wote ambaye maisha yake yote ya soka yamehusishwa na jina la klabu ya FC Barcelona. Ana mafanikio ya aina zote katika ngazi ya klabu na kilichobaki pekee ni mafanikio na timu ya taifa ya Argentin.
Mshambuliaji huyo alianza kuitumikia klabu ya FC Barcelona msimu wa 2004/05 na tangu wakati huo amekuwa akivunja kila aina ya rekodi na kuweka mpya.
Messi amevunja rekodi binafsi na za timu, akianza wakati alipofunga goli la kwanza baada ya mechi 7. Misimu 13 baadae, hivi sasa ndio mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo na yupo kwenye 3 bora ya wachezaji waliotumikia Barcelona kwenye michezo mingi zaidi.

Kukosa mafanikio na Argentina
Kitu pekee ambacho kinamuwekea wingu katika mjadala wa mwanasoka bora wa wakati wote ni kukosa mafanikio na timu yake ya taifa. Ameshashinda medali ya dhahabu ya Olympic 2008 jijini Beijing na medali ya Dhahabu ya kombe la
Dunia 2005, lakini amepoteza fainali mbili za Copa America, mara zote kwenye mikwaju ya penati dhidi ya Chile, na pia fainali ya Kome la dunia vs Ujerumani.
Lionel Messi vs Sevilla
Usiku wa leo Lionel Messi atacheza mchezo wa 600 akiwa na jezi za Blaugrana.
Leo anaingia dimbani kucheza dhidi ya timu ambayo ameifunga magolimengi zaidi katika maisha yake – Sevilla.
Mpaka sasa ameshacheza mechi 30 dhidi ya klabu hiyo ya La Liga, ameifunga magoli 29 na kutoa assists 10.
0 comments:
Post a Comment