Tunaelekea katika moja ya mapambano yanayovuta sana hisia za mashabiki siku ya leo ambapo Manchester United watakabiliana na Chelsea, lakini leo si mbaya ukapata kujua wachezaji 11 waliotumikia klabu hizi mbili.

11.Mark Hughes. Hughes alianza kucheza soka katika klabu ya Manchester United na baadae alikwenda Barcelona kisha Bayern na akarudi tena United huku mwaka 1995 akishinda kikombe cha Epl lakini Ferguson baadae akamuuza kwenda Chelsea alikoshinda FA na kikombe cha ligi.

10.Juan Sebastian Veron. Rekodi ya dau la £28.1m ilimpeleka United akitokea Lazio lakini baada ya misimu miwili tu ilipofika mwaka 2003 United walimuuza Veron kwa ada ya hasara dau la £15m ambako pia alishindwa kung’ara akapelekwa Inter Millan.
09.Ray Wilikins. Alianza kuitumikia Chelsea akiwa na miaka 17 tu hiyo ilikuwa mwaka 1973 lakini ilipofika mwaka 1979 Chelsea walikubali ofa kutoka United ya kiasi cha £800,000 wakamruhusu Wilikins kuondoka na kushinda FA mwaka 1983.

08.George Graham, huyu alizichezea timu kubwa tatu Epl Arsenal, Chelsea na United alianza kuichezea Chelsea mwaka 1960 akisainiwa kwa dau la £5000 kutoka Aston Villa na baadae akaenda Arsenal ambao ndio walimuuza kwenda Manchester United.

07.Paul Parker, moja kati ya walinzi bora wa kulia kuwahi kutokea Uingereza. Manchester United walimnunua kutoka Qpr na mwaka kati ya 1991 na 1996 akiisaidia United kubeba Epl 2, Fa 1 na kombe la ligi moja lakini majeruhi yakailazimu United kumuuza Chelsea.

06.Mal Donaghy, alikuwepo katika kikosi cha Manchester United kilichoshinda michuano ya Euro Super Cup mwaka 1991 lakini baada ya hapo United walimuuza kwenda Chelsea kwa dau la £100,000.

5.Mark Bosnich, aliisaidia United kuchukua kombe la Epl mwaka 1999 lakini mwaka mmoja baadae United walimuuza kwenda Chelsea ambako mwaka 2002 alifeli katika vipimo vya dawa za kutumia nguvu na kuondolewa Chelsea.
04.Radamel Falcao, wakati akitua United kutokea Monaco matumaini ya mashabiki yalikuwa makubwa sana lakini alionesha kiwango cha chini sana United ambao waliamua kumuacha aende Chelsea ambako nako aliboronga kabla ya kurudi Ufaransa
3.Juan Mata, kocha wa sasa wa Manchester United ndiye alimuuza Mata kutoka Chelsea kwa ada ya £37.1m akidai kwamba haendani na mfumo anaotaka yeye lakini sasa wote wanaitumikia Chelsea huku Mata na Mourinho wakiwa katika mahusiano mazuri.

02.Romelu Lukaku, Jose Mourinho tena alimtoa Lukaku kwenda West Bromich kwa mkopo na baadae alikwenda Everton kwa mkopo kabla ya Chelsea kumuuza mazima kwenda Everton na sasa yuko chini ya Mourinho Manchester United.

Matic,hapo kabla Mourinho hajaondoka Chelsea Matic alikuwa mchezaji wake kipenzi lakini ujio wa Antonio Conte ulibadili maisha ya Matic darajani na sasa yuko United.
0 comments:
Post a Comment