Timu
ya Arusha FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Bara, kupitia kwa Ofisa
habari wake Bahati Msilu wameliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
kufuta msimu wa Ligi Daraja la Kwanza 2019/20 kutokana na janga la
Virusi vya Corona linaloendelea kuitikisa Dunia.
Msilu
amesema:-"Ningefurahi kama ligi msimu huu ingehairishwa ili tuanze
kujiandaa kwa ajili ya msimu ujao kwani mapumziko haya ya kujikinga na
ugonjwa wa Covid-19 yametuharibia utaratibu wote kwani yametusababishia
gharama zisizokuwa za lazima maana tumetumia gharama ambazo hatukupaswa
kutumia kulingana na hali mbaya ya timu yetu kiuchumi tuliyonayo".
Msilu
aliendelea kwa kusema kama TFF wataruhusu ligi iendelee basi watoe
walau wiki mbili za kujipanga kila mchezo kutokana na hali mbaya
kiuchumi.
“
TFF kwa msimu huu wa 2019/20 wangeacha tujiandae kwa msimu ujao, ligi
ikiendelea ushindani utakuwa mdogo kwakuwa wachezaji wengi hawana
nidhamu ya kufanya mazoezi watarudi wakiwa wazito ukichanganya na janga
la Covid-19 hali ya uchumi imekuwa ngumu" , amesema.
0 comments:
Post a Comment