MSEMAJI wa klabu ya Simba, Haji Manara
amesema kuwa kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ ni mchezaji bora
Mtanzania katika nafasi ya kiungo licha ya kuwa bado hajaonesha uwezo
wake kwa asilimia 100.
Akizungumzia uwezo wa
kiungo huyo, Manara alisema kuwa Fei Toto anatakiwa kujitambua nini
anahitaji katika maisha yake ya soka, kwa kuwa amejaaliwa kipaji kikubwa
kuliko wachezaji wengi wazawa, lakini amekuwa akikwamishwa na vitu
vidogo vidogo ambayo anatakiwa kuvifanyia kazi mapema ili kufikia kwenye
kilele cha ubora wa asilimia 100.
“Fei Toto ni
moja ya kiungo aliyejaaliwa uwezo mkubwa uwanjani, ndiyo maana hata
kocha wa zamani wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike alimtabiria kuwa
atakuja kufanya makubwa zaidi kweye soka.
“Bado
hajatupa alichonacho kwa asilimia 100%, labda anahitajika kujua nini
kesho yake ijayo kwenye maisha ya soka, lakini kuhusu kabumbu yupo
vizuri na anaweza akafanya lolote akiwa na mpira katika miguu yake,”
aliandika Manara kwenye akaunti yake ya Instagram.
0 comments:
Post a Comment