Sunday, December 31, 2017


Na Priva ABIUD.
Ni miaka 6 imepita tokea mkurugenzi wa zaman wa Ac Milan bwana Adriano Galliani afanye kosa aliloliita kosa lake la maisha. Ni pale alipomruhusu kiungo bora kabisa Andrea Pirlo kujiunga na mahasimu wao wakubwa Juventus.  Kosa alilolifanya Gallian kwa sasa linamtesa mkurugenzi mkuu wa Millan kwa sasa Marco Fassone ambaye ameingia mgogoro mkubwa na Wakala wa Golikipa wa klabu hiyo Gianluigi Donnarumma kwa kila kinachoitwa vita ya pesa.  Donnaruma anahitaji kuondoka.
 Donnarumma mlinda mlango kwa Ac Milan  kwa sasa anaishi kama mkimbizi ndani ya taifa lake. Hivi majuzi tu kwenye mchezo wa  timu taifa ya vijana ya Italia Donnarumma alitupiwa hela feki na mashabiki kwa kile walichodai kuwa bwana mdogo aligomea mshahara wa E80,000 kwa wiki akiwa na miaka 18 tu. Mino Raiola aliyekuwa dalali wa dili la Paul Pogba, ndiye wakala wa Donnarumma, na alikanusha kuwa mteja wake kuwa hakusaini kwa sababu za kifedha. Raiola ilisema alihofia usalama wa mteja wake klabuni hapo. Donnaruma alijiunga Ac milan akiwa na miaka 16 akiwa anapata mshahara wa E100,000 kwa mwaka.
Amejipatia umaarufu mkubwa kwa uwezo wake akiwa golini. Baada ya sekeseke kuisha Donna alisaini mkataba mpya ambapo alikuwa akipokea Euro milion 6 kwa mwaka. Lakini bado inaonekana ugonjwa ule umerudi tena. Mino Raiola anamwekea kijana huyu mazingira magumu sana. Mino amesikika mara kadhaa akilalamika kuwa Donnarumma haheshimiki na baadhi ya Vipengele vya mkataba wake havilindwi.
Donnaruma alisaini mkataba mpya mpaka 2012. Pia Ac Milan ilimsajili kaka yake. Kivumbi kilianza kwenye mchezo wa Copa Italia dhidi ya Verona ambapo mashabiki uwanja mzima walikuwa wakimzomea. Donnarumma alijikuta akitoa machozi San Siro. Mashabiki wa Ac Milan ni wakorofi sana. Hawana uvumilivu. Wamekosa uvumilivu wa kisoka. Bado chuki za kuporomoka kwa soka lao linawapa stresi. Inafika steji wanaanza kuwatukana hadi wachezaji wao wazawa wanapotaka kulinda maslahi yao.
Mashabiki wamekaa kwenye viti na mabango kumzomea mtu aliyejitolea maisha yake kulinda furaha yao lakini bado wanamtukana. Walio wengi wanamtukana Donnaruma wanasema kuwa anapenda hela kuliko klabu ya Ac Milan.
Kwa akili ya kawaida ni nani hapendi pesa? Yuda Iskarioti mwenywe alimuuza Mwana wa Mungu kisa pesa. Makanisa mengi duniani yanahimiza matoleo ya sadaka, wewe ni nani kama viongoz wa dini wanatuhubiria kuhusu sadaka? Hivi unajua kazi anayoifanya Donnaruma pale golini? Yaani mtu anajitupa kufuata mashuti ya watu mnasema anapenda hela? Mlitaka apende nini? Cha muhimu katika maisha ya mchezaji kwanza ni maslahi yake. Huwezi kutegemea kazi ya mchezaji bila kutimiza maslahi yake.
Nawashangaa sana Mashabiki wa Ac Milan ambao  wamepoteza muda wao wakizunguka mitaa ya Santa Maria Dele gracie kwenye steshenari za Fabriano Boutique, Pettinaroli na wengine wakijazana maduka ya San Maurilio na Pasini Milano kutengeneza hela bandia ili wakamtupie Donnoruma.
Kwan wanadhani Donnarumma hapendi maisha mazuri? Hivi ni kweli kwamba hapendi kutembelea Buggati Veryon na kupumzika hoteli za kifahari kama  Pallazo Parigi kule milano? tena kwenye vyumba vya gharama kabisa? Nae  anapenda kwenda fukwe za Puglia na San Vitolo Capo kule sicily kula bata wakati wa mapumziko na familia yake. Yaani kwa akili yao wanafikiri Donnarumma anapopigiwa mashuti golini na kudaka kama mtu asiye na akili kwamba hawazi maisha mazuri?  KAMA DONNARUMA ATAKUBALI KUONDOKA NDANI YA TAIFA LAKE ATAJIJENGEA UADUI MKUBWA SANA KWA WAITALIANO NA ATAPOTEZA HESHIMA YAKE. ACHAGUE POCHI LA RAIOLA AU MAKOFI YA HESHIMA SAN SIRRO. Narudia tena heshima zipo jeshini kwenye soka cha kwanza maslahi. Siku njema

Comments

0 comments:

Post a Comment