Rais wa shirikisho la soka barani Afrika Ahmad Ahmad wakati
anaingia madarakani aliahifi mabadiliko kiutendaji lakini pia katika
maeneo mengine ya ambayo yanagusa mambo ya kiufundi kama mashindano na
mambo mengine ambayo yapo chini ya shirikisho hilo.
Miongoni mwa mabadiliko ambayo Ahmad Ahmad aligusia ni namna ya
kumpata mchezaji bora wa Afrika, January 4, 2018 mchezaji bora wa Afrika
atachaguliwa. Mfumo uliozoeleka awali ilikuwa ni kwamba, makocha na
manahodha wa timu za taifa ndio walikuwa na jukumu la kuchagua (kupiga
kura) kwa ajili ya mchezaji bora wa bara la Afrika.
Kwa sasa shirikisho la soka Afrika limeongeza kipengele kingine cha
kumpata mchezaji bora wa Afrika, ukiacha makocha pamoja na manahodha wa
timu za taifa, wadau kwa maana ya mashabiki, watakuwa na fursa ya
kuchagua mchezaji bora wa bara la Afrika.
Ni mabadiliko mengine ambayo tunayashuhudia chini ya Ahmad Ahmad
kutokana na sera yake wakati anaingia madarakani kwamba mabadiliko ni
lazima kwa shirikisho la soka Afrika.
Wachezaji ambao wameingia fainali kuwania tuzo ya mchezaji bora Afrika ni Mohamed Salah, Sadio Mane na Pierre-Emerick Aubameyang
Home
»
»Unlabelled
» Mashabiki kuamua mchezaji bora Afrika
Wednesday, December 27, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment