
Image caption Adrien Silva alitajwa kwenye benchi wakati wa mechi dhidi ya Huddersfield uwanjani King Power
Kiungo wa kati wa
Ureno Adrien Silva hatimaye amefanikiwa kuhamia Leicester City, baada ya
kushindwa majira ya joto klabu hiyo ilipochelewa kuwasilisha nyaraka
zake kwa sekunde 14.
Fifa walikataa kuidhinisha uhamisho wa
mchezaji huyo wa miaka 28 kutoka Sporting Lisbon wakati huo wakisema
muda wa kuhama wachezaji ulikuwa tayari umepita.Mreno huyo amekuwa akifanya mazoezi na Leicester kipindi chote cha majira ya joto kuimarisha kiwango chake cha uchezaji.
Uhamisho wake wa £22m ulikamilishwa Jumatatu na akatajwa kwenye benchi mechi ya Leicester nyumbani dhidi ya Huddersfield.
Silva, ambaye ni mzaliwa wa Ufaransa, alitoka akademi ya Sporting Lisbon, na amekuwa kwa mikopo Maccabi Haifa na Academica.

Silva amesema alipitia kipindi kigumu sana miezi hiyo minne akisubiri dirisha lifunguliwe tena Januari, lakini amekuwa akitia bidii kujiweka sawa kucheza.
Hayo yakijiri, Leicester wamemuita tena kiungo wao Harvey Barnes kutoka Barnsley alikokuwa kwa mkopo tangu Agosti.
0 comments:
Post a Comment