Maneno ya Mwana FA yanakuja baada ya United kuwapiga Everton mabao mawili yanayowarudisha hadi nafasi ya pili ushindi unaowafanya United kuifunga Evrton mara 35 idadi kubwa zaidi kuifunga katika EPL
Alikuwa ni Anthony Martial alifunga bao la kwanza linalomfanya kuifunga Everton mabao 4 katika mechi 6 dhidi yao huku Jesse Lingard akifunga lingine linalomfanya kuwa mchezaji wa pili United kufikisha mabao 10 msimu huu.
Katika
matokeo ya mapema klabu ya Liverpool imeendeleza wimbi la matokeo
mazuri baada ya Sadio Mane na Ragnar Klavan kuwapatia Liva mabao mawili
ambayo yamewafanya kuibuka kidedea na ushindi wa bao mbili kwa moja.
Sasa
Manchester United wanasubiria matokeo ya mchezo kati ya Arsenal na
Chelsea utakaopigwa siku ya Jumatano ambapo kama Chelsea atapigwa
watabaki nafasi ya pili lakini Chelsea akishinda wataishusha United.

0 comments:
Post a Comment