MTOTO
wa Rais wa wa Liberia, George Weah aitwaye Timothy 'Tim' Weah akiwa na
umri wa miaka 18 jana ameichezea kwa mara kwanza timu ya taifa ya
wakubwa ya Marekani katika ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki
dhidi ya Paraguay.
Tim anafuata nyayo za baba yake, Weah ambaye ni Mwanasoka Bora wa Dunia wa FIFA mwaka 1995, anayekuwa mchezaji wa kwanza aliyezaliwa miaka ya 2000 kuichezea timu ya wakubwa ya Marekani.
"Hiki ndicho nimekuwa nikikisubiri kwa maisha yangu yote. Nimeheshimu sana nafasi niliyopewa ne benchi la ufundi la makocha, na ninatumaini kwamba nitaitwa zaidi",alisema.
Tim Weah jana ameichezea Marekani mechi ya kwanza ikishinda 1-0 dhidi ya Paraguay PICHA ZAIDI GONGA HAPA

Kinda
huyo aliingia dakika ya 86 akitokea benchi Alfajiri ya leo katika
mchezo ambao bao la penalti la Bobby Wood dakika ya 45 liliipa ushindi
wa kwanza Marekani katika mechi tatu chini ya kocha wa muda, Dave
Sarachan.
Weah
alicheza mechi ya kwanza kikosi cha timu ya taifa ya wakubwa ya Paris
Saint-Germain Machi 3, kiasi cha wiki mbili baada ya sherehe za kutimiza
kwake miaka 18 ya kuzaliwa.
Alicheza
pamoja na kiungo, Mmarekani mwenzake, Darlington Nagbe, ambaye baba
yake, Joe alikuwa Nahodha wa Liberia na mchezaji mwenzake, George Weah.
Sarachan,
ambaye alichukua nafasi ya Bruce Arena baada ya Marekani kukosa tiketi
ya Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018, aliwapongeza vijana wake kwa
ushindi huo.
Kikosi
cha Marekani kilikuwa; Steffen, Yedlin, Miazga, Adams, Carter-Vickers,
Nagbe/Roldan dk90, Wood/Novakovich dk77, Delgado/Weah dk86, Saief/Rubin
dk67, Villafana na Trapp.
Paraguay:
Fernandez, Gomez, Balbuena, Valdez, Camacho/Perez dk55, Rojas/Gonzalez
dk81, Santander, Alonso, Riveros/Ortiz dk66, O. Romero/Dominguez dk81 na
Almiron.

0 comments:
Post a Comment