Beki
Marcos Rojo akikimbia kushangilia kishujaa huku amedandiwa mgongoni na
Nahodha wake, Lionel Messi baada ya kuifungia Argentina bao la ushindi
dakika ya 86 ikiilaza Nigeria 2-1 katika mchezo wa mwisho wa Kundi D
Kombe la Dunia leo Uwanja wa Saint-Petersburg nchini Urusi. Argentina
ilitangulia kwa bao la Messi dakika ya 14, kabla ya Victor Moses
kuisawazishia Super Eagles kwa penalti dakika ya 51, kufuatia Javier
Mascherano kumshika hadi kumungusha Leon Balogun kwenye boksi wakati wa
kona. Lakini refa Cuneyt Cakir aliingia lawamani kwa kuwanyima penalti
ya pili Nigeria, huku Argentina ikienda hatua ya 16 Bora kama mshindi wa
pili wa kundi kwa pinti zake nne nyuma ya Croatia, iliyomaliza na
pointi tisa. Argentina itamenyana na Ufaransa Juni 30, wakati Croatia
itamenyana na Denmark Julai 1
Home
»
»Unlabelled
» ROJO AIPELEKA ARGENTINA 16 BORA, KUIVAA UFARANSA JUNI 30
Wednesday, June 27, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment