“Its Coming Home” hayo ndio matumaini ya Waingereza msimu huu
wa kombe la dunia, Uingereza wanaona hii ni nafasi yao kwa kurudisha
kombe nyumbani na matumaini zaidi ni baada ya ushindi wa jana vs
Colombia.
Harry Kane bado anaonekana kuibeba Uingereza, baada ya jana kuifungia
bao kwa mkwaju wa penati ambalo linakuwa bao lake la 6 msimu huu wa
kombe la dunia akiendelea kukaa kilele cha ufungaji.
Mwaka 1939 katika kombe la dunia Tommy Lawton alifunga mara 6
mfululizo kombe la dunia, na bao la jana la Kane linamfanya kuvunja
rekodi ya Lawton iliyodumu kwa miaka 79.
Kama hiyo haitoshi, Harry Kane tena amevunja rekodi ya Hristo
Stoichcov raia wa Bulgaria aliyoweka mwaka 1994 ya kufunga penati 3
tofauti katika msimu mmoja wa michuano ya kombe la dunia.
Ni wachezaji watatu tu Sandro Kocsis(9), Gerad Muller(7) na Guillermo
Stabile (7) ndio ambao wamewahi kufunga idadi nyingi ya mabao kuliko
Harry Kane(6) katika mechi zao 3 za mwanzo kombe la dunia.
Alan Shearer mwaka 1998 vs Tunisia alikuwa mchezaji wa mwisho
kufanyiwa faulu nyingi katika mechi moja(faulu 11), na jana Kane
alipigwa kiatu mara 9 hii inamfanya kukaa katika nafasi ya pili.
Na kama haujui tu ni kwamba Harry Kane huyu huyu amefunga mabao 6
katika mashuti 6 aliyolenga lango, na hii ina maana kila shuti alilopiga
golini kwa wapinzani lilizaa bao.
Na kwa ujumla (hadi out of target) Kane amepiga mashuti 9 kupata
magoli 6 kombe la dunia, Wakati Neymar alipiga mashuti 38, Lionel Messi
67 na Cristiano Ronaldo mashuti 74 kufikisha mabao hayo.
Home
»
»Unlabelled
» Kuelekea Robo Fainali, Harry Kane ndiye mchezaji tishio zaidi Urusi
Wednesday, July 4, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment