Nahodha
wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta anayecheza
katika klabu ya KRC Genk ya Belgium na mshambuliaji wa Al Hilal ya Sudan
Thomas Ulimwengu wametua nchini leo alfajiri kujiunga na kambi ya timu
hiyo inayojiandaa kuivaa Uganda wikiendi hii jijini Kampala.
Stars
inajiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon dhidi ya
Uganda, mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka wa
Tanzania na Uganda.
Wachezaji
wengine wanaokipiga nje ya Tanzania ambao wamejiunga na kambi hiyo ni
pamoja na Rashid Mandawa anayekipiga nchini Botswana na Ramadhani Kessy
anayetokea nchini Zambia.
0 comments:
Post a Comment