Kumekuwa na taarifa kuwa uongozi wa Yanga unavutiwa na beki Rwabutaye Abdoul kutoka Rayon Sports.
Lakini
mmoja wa viongozi wa Yanga amesema kuna mchezaji wa Rayon ambaye
wanaamini atawasaidia baadaye na Abdoul ndiye amekuwa wakimtumia kumpata
mchezaji huyo.
“Ni
kweli Abdoul ni mchezaji mzuri lakini ana mkataba na Rayon, sisi
tunachofanya ni kupambana kumpata mchezaji mwingine wakati wa dirisha
dogo.
“Abdoul
atakuwa anatusaidia, mara atakapomaliza mkataba basi tutapambana
kumnasa. Lakini nafikiri wengi hawajaelewa, wanadhani tunamtaka Abdoul,”
alisema.
Kulikuwa na mgogoro mkubwa wakati beki huyo akitua Rayon kutoka APR na klabu hizo mbili ni wapinzani wakubwa.
Lakini
wakati Yanga wakisema hawana mpango na Abdoul, tayari uongozi wa Rayon
Sports umesisitiza, beki huyo Mnyarwanda ana mkataba.
Katika
tofuti ya Rayon Sports, imeonyesha klabu yoyote inayotaka kumnasa
Abdoul au mchezaji mwingine wa Rayon mwenye mkataba, itakuwa matatizoni.
Rayon
Sports imesonga mbele katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho
ikiwa na USM Alger ya Algeria huku Yanga na Gor Mahia zikiondolewa.
0 comments:
Post a Comment