TIMU
ya Esperance imetwaa ubingwa wa klabu bingwa Afrika kwenye mchezo wa
fainali ya pili dhidi ya Wydad Casablanca baada ya Wydad kugoma
kuendelea na mchezo huo dakika ya 62 kwa kutokubaliana na maamuzi ya
mwamuzi.
Kwenye
mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa, Wydad walisawazisha bao
walilofungwa na mwamuzi akalikataa kwa kudai wameotea jambo ambalo
wachezaji hawakukubali na kuomba mwamuzi akatazame VAR ili kujiridhisha.
Waamuzi
wa mchezo huo hawakujua kwamba VAR ni mbovu hivyo walipotoa taarifa
hiyo wachezaji wa Wydad wakaamini kwamba wanaonewa makusudi kwani mchezo
wao wa kwanza mwamuzi aliyewaamua alifungiwa na Caf kwa kuchezesha
chini ya kiwango.
Licha ya jitihada za Rais wa Caf, Ahmad Ahmad kuzungumza na mabosi wa pande zote hazikuzaa matunda.
Refa
wa kati aliwaamuru warudi uwanjani wakagoma kurejea uwanjani na kwenda
kwenye vyumba vya kubadilishia nguo hali iliyofanya mabingwa kutangazwa
kuwa Esperance.
Wydad
wanaamini kwamba bao lao la kusawazisha dakika ya 59 lililofungwa na
Walid el Karti na kuzama wavuni lilikuwa halali hivyo hawana imani na
mwamuzi.
Hii
inakuwa ni mara ya kwanza kwa mchezo wa fainali kushindwa kumalizika
baada ya miaka 55 ya historia ya mashindano ya Afrka kwenye michezo ya
nyumbani na ugenini.
0 comments:
Post a Comment