
Miamba ya soka
Uhispania klabu ya Barcelona imemsajili msahmbuliaji wa Ufaransa Antoine
Griezmann kutoka klabu pinzani ya Atletico Madrid kwa kitita cha euro
milioni 120.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 alikuwa sehemu ya
kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kilichonyakua kombe la dunia mwaka
jana. Griezmann ameingia mkataba wa miaka mitano na Barcelona ambao umeweka sharti la euro milioni 800 kwa klabu yeyote itakayotaka kumng'oa Nou Camp.
Mshambuliaji huyo machachari alijiunga na Atletico akitokea Real Sociedad mwaka 2014 na ameifungia Atletico magoli 133 katika michezo 256.
- Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 12.07.2019
- Kivumbi kutifuka nusu fainali ya Afcon
- Sturridge ampata mbwa wake aliyepotea
Griezmann sasa anakuwa mchezaji wa sita ghali zaidi duniani kusajiliwa nyuma ya Neymar, Kylian Mbappe, Philippe Coutinho, Joao Felix na Ousmane Dembele.
Ameshinda mataji kadhaa na Atletico kama Kombe la Europa, kombe la Super Cup la Uhispania, pamoja na Uefa Super Cup.
Pia amekuwa kinara wa magoli wa klabu hiyo katika misimu mitano iliyopita klabuni hapo.
Griezmann anakuwa mchezaji wa nne mkubwa kusajiliwa na Barcelona katika dirisha hili la usajili baada ya kiungo Frenkie de Jong kutoka Ajax, golikipa Neto kutoka Valencia na beki Emerson kutoka klabu ya Atletico-MG ya Brazil.
Usiyoyajua kuhusu Griezmann?
- Alikataliwa kwenye vilabu vya watoto kwa kuwa na umbo dogo sana.
- Griezmann ni mpenzi wa ligi ya kikapu ya NBA na mchezaji anayempenda zaidi ni Derrick Rose wa Detroit Pistons.
- Nyumba yake jijini Madrid ina uwanja wa mpira wa kikapu
- Mfaransa huyo ni mpenzi wa taifa la Uruguay na tamaduni zake na amevutiwa zaidi na wachezaji wenzake kutoka taifa hilo
Utata wa usajili na safu kali ya ulinzi ya Barca
Griezmann baada ya hapo akaikataa ofa ya kuhamia Barcelona mwaka jana, lakini mwanzoni mwa mwezi huu Atletico ikatoa malalamiko tena juu ya jambo hilo.
Klabu hiyo iliishutumu Atletico na Griezman kwa utovu wa adabu kwa kuafikiana juu ya uhamisho bila kufuata njia rasmi.
Griezmann ni nyota watatu kuihama Atletico msimu huu baada ya beki Lucas Hernandez kujiubga na Bayern Munich na kapteni wa muda mrefu wa klabu hiyo Diego Godin kuhamia Inter Milan baada ya kwisha kwa mkataba wake.
Klabu hiyo pia imetumia kitita cha euro 126 kumnunua Felix kutoka Benfica.
Atletico ilimaliza katika nafasi ya pili msimu ulipita nyuma ya Barcelona kwa alama tisa.
Griezmann, ambaye alikuwa wa tatu katika tuzo za Ballon d'Or kwa mwaka 2016 na 2018, anaungana na Lionel Messi, Luis Suarez na Dembele katika safu 'hatari' ya ushambuliaji ya Barcelona.
0 comments:
Post a Comment